Showing posts with label Nasadiki.. song. Show all posts
Showing posts with label Nasadiki.. song. Show all posts

Thursday, 26 November 2015

Naondoka Mimi

Naondoka  Mimi  naenda  kwa baba,  nipeleke  hiki  nilichokipata,
Japo kidogo sijaona haha, nimekua sitarudi  nyuma. 

   Chorus :
.nakuja  polepole  mimi  nakuja  na zawadi  (yangu)
Naletaa  mbele  zako  Ili  nitoe  shukurani.

Stanza  two :
Natembea  mimi mwendo  WA  madaha, nakanyanyanga  Chini  kwa maringo  Tele, naelekea  altari  ya  Bwana  nimkabidhi  nilichojaliwa.

Stanza  three :
Nimechangamka ninamshangilia, napiga  kelele, kelele  Za  shangwe, nacheza  cheka najongea  kwako , we Mungu , eh  Mungu  Baba  nipokee  mimi.

Stanza  four :
Nafsi  yangu  mimi  naileta  kwako, mkate divas, pia  ninaleta, uigeuze  mwili  na damu  ya  chakula chetu tunaosafiri.

Stanza  five :
Mavuno  shambani  mimi  nimevuna, mifukoni  fedha nimebarikiwa.
Mimi ni Nani  nisishukuru.,  Baba  nasema  Asante  kwa  yote..