Monday 7 March 2016

MAMBO YABADILIKA LYRICS BY HELLENA KEN

Huu, ni mwaka wa urejesho x2
Mambo, mambo yabadilika x2 (Repeat)

(CHORUS)
Naona mambo yakibadilika
(Yabidilika kwa wema wako) (REPEAT)

Mambo, mambo yabadilika x2

Walio chini sasa, naona wakiinuliwa
Walio nyuma sasa, naona wakiwa mbele Wanaodharauliwa, naona heshima zao Wanaolia sasa, machozi yanapanguzwa

Huu ni mwaka wa urejesho x2 Uliyepoteza ndoa, naona ikirejeshwa Uliyepoteza watoto, naona wakirejeshwa Uliyepoteza nyumba, naona ikirejeshwa Uliyepoteza kazi, naona ikirejeshwa Uliyepoteza cheo, naona kikirejeshwa Uliyepoteza heshima, naona ikirejea Kwani mambo yabadilika

(CHORUS)
Majina yaenda kubadilika x2
Wanaoitwa tasa, naona wakiitwa mama Wanaodharauliwa, naona heshima zao Wanaoitwa duni, sasa wainuliwa Walio pekee yao, waenda pata wachumba
Kwani mambo, mambo yabadilika x2 Wanaolia sasa, machozi wanapanguza Waliokataliwa, sasa wakubalika
Wasio na makao, wapata makao yao
Walio na  huzuni wapata amani yao
Wasio na furaha, wapata furaha yao Kwani mambo, mambo yabadilika x2

(CHORUS)
Jipe jina, tutakuita unapojiita sasa
Pokea jina jipya, maana majina yabadilika

Refrain:
Naitwa mbarikiwa
Tukuite nani nani leo Jipe jina, jipe jine
Na wewe waitwa nani leo Baba yangu tukuite nani Jipe jina, jipe jine
(CHORUS)

No comments:

Post a Comment