USIFURAHI JUU YANGU Lyrics by Upendo Nkone
Usifurahi juu yangu eeeh adui yangu Niangukapo mimi nitasimama tena Kumbuka niwapo gizani bwana ni nuru yangu
Hawezi kuniacha bwana mimi niangamie ×2
Si vyema kunisema vibaya nipatapo tatizo Shetani wampa nafasi ndani ya moyo wako
Kumbuka kwa maombi yako nitasimama tena
Na utapata baraka kutoka kwake mungu ×2
Maana heri mtu yule ambaye kinywa chake Ni kuwabariki wenzake na kiwaombea
Maana maneno mabaya huchafua moyo Ukiwekwa mbali na mungu ni vyema uwe safi
Ukiona niko kwenye shida niombee
Ndoa yangu imevunjika wewe niombee Nikifukuzwa kazini ndugu niombee Magonjwa yananiandamaa niombee Biashara haina faida niombee
Nikikawia kupata mtoto niombee Nimekuwa mtoto yatima niombee
Ata nijapo kuwa mjane niombee
Ujue kwa maombi yako mimi nitasimama tena
Ujue kwa maobi yako nitabarikiwa ×4
No comments:
Post a Comment