MAPITO lyrics by Gloria Muliro Ehhhhhahh Ehhhhahhh Ehhh
Mimi nashangaa kumbe wakati wa mapito, mambo yote hubadilika (hmm)
Mimi nashangaa kumbe wakati wa mapito, ata rafiki anakutoroka
Mimi nashangaa kumbe wakati wa mapito, hauna wa kukutia moyo
Jamani nashangaa kumbe wakati wa mapito, mambo yote hubadilika
(mm)
Hizi miaka zote mpenzi tumekuwa tu vizuri, lakini kuanza jana unabadilika (ooh)
Hutaki kuniona kunikaribia, hutaki mpenzi Pesa unasema kwamba sinanga pesa Hizi miaka zote mpenzi,
leo ndio umefunguka macho umeona kwamba mimi masikini sinanga pesa
Afadhali uniache jinsi ulivyonipata
Najua ni mapito tu Bwana ananishughulikia
Nasema siwezi kumwacha mungu wangu juu yako penzi Mungu wangu ananishughulikia tu eheh
(CHORUS)
Uchungu wa mwana ni mzazi aijuaye Mapito yangu, baba wa mbingu anaona ×2
Jamani wakati wa mapito, mapito wo Usingojee kupigiwa makofi,bali kupigwa makofi
Jamani wakati wa mapito, usitarajie kutiwa moyo, bali kuvunjwa moyo
Wakati wa mapito, mapito wo usitarajie marafiki bali manafiki kibao ooh
Utakapopata kesho, wengine wao watakurudia aah
Watasema wanakujua,
watasema walisimama na wewe ah usiwakemee..
Mungu, mungu ndiye analipa yeee Uchungu wa mwaanaa....
(CHORUS)
No comments:
Post a Comment