Thursday 26 November 2015

Vipaji tumepewa

stanza one.
Vipaji  tumepewa, mapato  tumepata  lakini  binadamu  tunashindwa  kushukuru
Wakati  tunaomba  tunajinyonyekeza lakini  tumepata mikono  yetu  birika.

Chorus :
Mpeni  kaisari  yaliyo  yake ;mpeni Mungu  yaliyo  yake  Mungu *2

Stanza two.
Mifugo  tunafunga  nafaka  tunavuna  lakini  kila  siku tunakula  na kusazo;
Kumbuka  Kuna  wale  wasio  na chochote  hawawezi  kupata  hata  kikombe  cha  maji..

Stanza  three.
Tunapofanya  kazi  twapata  mishahara, shughuli  zetu  kwanza  kuingia  kwenye  baa;
Ikiwa  zitabaki, twakuja  kanisani  twamtolea  Mungu  shilingi  moja  na tano.

Stanza  four :
Tukiwa  na  wagonjwa  hatuwasaidii  Wakati  wamekufa  tunachanga  kwa huzuni ;
Twachukua  mikopo  kwa  mambo  ya  anasa, ujenzi  wa  kanisa  twalazimishwa  kutoa.
.
Stanza  five :
Kumbuka  Ibrahim  alimtoa  mwanao  kama  sadaka  tosha  kwake  Mungu  WA  mbinguni ;
Na sisi  kwa  furaha  tupeleke  sadaka  itayopendeza kama Ile  ya Abeli.

No comments:

Post a Comment