Thursday 26 November 2015

NYANYUKENI

(*2Nyanyukeni  waumini  wote  tufanye  shangwe, kwa  nderemo  kwa vigelegele  na kwa  vifijo) *2(Bwana asifiwe (sana) Bwana  asifiwe (kweli)  Bwana  asifiwe. Mwathani  arogocwo) *2.
Stanza  one :
Nikiziangalia  Mbingu  ni  kazi  ya 
Vidole  vyako, mwezi  na nyota  Za mbinguni  ulioratibisha  wewe.

Stanza  two
Uwezo  wake  Bwana  Mungu 
Haupimiki kwa  mizani , mipango
Yake  kwetu  sisi  haiweziii  kubadilishwa.

Stanza  three ;
Alikausha  bahari  ya sham  ikawa  nchi
Kaku,  waisraeli  wakapita  kwa  Uwezo
Wa  Mungu  Baba 

Stanza  four.
Na tupigeni  tarubeta  kinubi  hata  na
Matari, tuimbe  wimbo wake  Musa na
Ule  wa  mwanakondoo.

Stanza  five.
Tupazeni  sauti  kwa  shangwe 
Hata  vifijo , Sifa  pia  na  utukufu  tumpe  Bwana  siku  zote.

No comments:

Post a Comment