Sunday 20 December 2015

Eeh BWANA UMENICHUNGUZA LYRICS BY CHRISTINA SHUSHO

Christina Shusho - Ee Bwana Umenichunguza

Lyrics in Swahili

Christina:
Ee bwana umenichunguza,
nakunijua Wewe wajua kuketi kwangu,
na kuondoka kwangu
Umelifahamu wazo langu,
        tokea mbali
Umepepeta kwenda kwangu, na kulala kwangu Umeelewa na njia zangu zoote
Umepepeta kwenda kwangu, na kulala kwangu Umeelewa na njia zangu zoote
      Aaah uuuh mmmh
Maana hamna neno uilmini mwangu,
usilojua kabisa Bwana
Umenizingira nyuma na mbele,
ukaniwekea mkono wako
Maarifa haya ni ya ajabu,
yanishinda mimi,
hayadhihiriki Siwezi kuyafikia,
hayadhihiriki, Siwezi kuyafikia

Niende wapi nijiepushe,na Roho yako
Niende wapi niukimbie uso wako
Kama ningepanda mbinguni wewe uko Ningefanya kuzimu kitanda, huko nako uko Kama nikisema hakika giza litanifunika,
Giza nalo halikufichi kitu,
Giza na mwanga kwako ni sawasawa

Ee Mungu unichunguze,
ujue moyo wangu Ee Mungu
    (Ee Mungu eee)
Unijaribu, uyajuwe mawazo yangu
       Eeh Mungu (Ee Mungu)
Eeh Mungu (Uone kama)
Uone kama niko njia iletayo majuto ndani yangu
      (Eeh Mungu ee) Eeh Mungu
      (Ukaniongoze)
Ukaniongoze katika njia ya haki
      (mileeele)
milele (maana wewe) Maana wewe ndiwe uliye niumba
     (uzima wangu)
Uzima wangu (Eeh Mungu ee) Ee Mungu                  ( macho  yako)
Macho yako yaliniona kabla sijakamilika
    (eeh Mungu ee)
Ee Mungu (Nimekuita)
Uisikie sauti yangu (Nikuitapo baba)

Eeh Mungu (Eeh Mungu Ee)
Ee Mungu (Ee Mungu)

Ee Mungu unichunguze, ujue moyo wangu Ee Mungu
      (Ee Mungu eee)
Unijaribu, uyajuwe mawazo yangu
     Eeh Mungu (Ee Mungu)
Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo Yapate kibali mbele zako Eeh Mungu
       (Ee Mungu) Eeh Mungu
Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo Yapate kibali mbele zako
   Eeh Mungu Eeh Mungu
Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo Yapate kibali mbele zako Oooh ooh
     Eeh Mungu, Eeh Mungu

5 comments:

  1. Dope song.....just love it...it makes me feel God's presence

    ReplyDelete
  2. Still the best song for me when I'm blessed, when I'm down, when I'm happy when I am sad when I am blessed.

    ReplyDelete
  3. "...Maneno ya kinywa changu na mawazo ya Moyo yapate kibali mbele zako...Blessings2021

    ReplyDelete

  4. Blessings, I thank God for you shush

    ReplyDelete