ENDA NASI LYRICS BY SIFA VOICES KENYA
Tunaomba uwepo wako uende nasi,
Ewe bwana wa majeshi tusikie,
Kama uendi nasi hatutaki kutoka hapa, Hatuwezi peke yetu enda nasi
Tu watu wa shingo ngumu tusamehe, Hatufai mbele zako turehemu,
Tusafishe baba, tuonyeshe uso wako, Twahitaji neema yako enda nasi,
Tutavua, mapambo yetu,
Vitu vyote vya dhamani kwetu,
Mioyo yetu twaleta mbele zako,
Tutakase na utembee nasi,
Tunaomba utuonyeshe njia zako,
Kwa maan umetuita kwa jina lako,
Twalilia e bwana, utukufu na uso wako, Bila wewe tutashindwa enda nasi,
Tutavua, mapambo yetu,
Vitu vyote vya dhamani kwetu,
Mioyo yetu twaleta mbele zako,
Tutakase na utembee nasi,
Ndugu na dada yangu,
tafadhali usijaribu kuyamudu maisha bila yake bwana, utashindwa
Yafaa tufike mahali ambapo musa alimlilia bwana na kutafuta uso wake,
na kusema bwana tafadhali, enda nasi, enda nasi, twakuhitaji.
Tutavua, mapambo yetu,
Vitu vyote vya dhamani kwetu,
Mioyo yetu twaleta mbele zako,
Tutakase na utembee nasi X2
Mioyo yetu twaleta mbele zako,
Tutakase na utembee nasi
No comments:
Post a Comment